Rais wa Jamhuri ta Tanzinia Dkt John
Magufuli, ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu
katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia
sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo nchini humo.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo hii leo katika Ikulu ya mjini Dar es Salaam,
muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna mkuu wa mamlaka ya kupambana na
kuzuia dawa za kulevya Bwana Rogers Siyanga, Kamishna Jenerali wa
uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji
Mheshimiwa Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mheshimiwa
Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanznia nchini Uganda Mheshimiwa Grace
Aaron Mgovano.Rais Magufuli asikitishwa na gharama ya ujenzi, uwanja wa ndege
Mihadarati: Polisi 12 wasimamishwa kazi Tanzania
#Dkt Magufuli amewataka viongozi wote wa serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.
Mheshimiwa Magufuli amrwapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya, na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudu za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya, ambazo zinazidi kuangamiza nguvu kazi ya taifa.
No comments:
Post a Comment