Sadio Mane ndiye aliyepeleka majonzi kwa kikosi cha Pochettino kilichocheza chini ya kiwango, Tottenham bado inashika nafasi ya pili kwenye msimamo
Spurs hawakuweza kuipa presha yoyote Chelsea ambayo ni kinara wa Ligi hadi sasa baada ya kuangukia pua kwa kipigo hicho kwa mabao mawili yaliyokwamishwa kambani na Sadio Mane, na kumwacha Pochettino akiomboleza.
"Walikuwa bora zaidi yetu na walistahili kushinda. Tulianza mchezo hovyo kabisa" alisema Pochettino kwa mujibu wa BBC Sport.
"Ni vigumu kuelewa, nilivunjwa moyo sana na kiwango chetu cha kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili tuliweza kukabiliana nao lakini tulikuwa tumechelewa. Timu yote ilikuwa dhaifu. Leo tumecheza chini ya kiwango, huo ndio ukweli.
"Tupo kwenye nafasi ambayo tutajilaumu wenyewe. Lakini kama tukiendelea kucheza kama ilivyokuwa leo, hatutaweza kuendana na presha ya michuano na itakuwa ngumu kupambana kutwaa taji.
"Katika dakika 45 tuliona timu ambayo haikuwa tayari kupigana kwa ajili ya taji la Ligi Kuu."
Tottenham bado inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, lakini wanaweza kujikuta pointi 12 nyuma ya Chelsea iwapo wataifunga Burnley Jumapili mchana.
No comments:
Post a Comment