Mamlaka katika baadhi ya maeneo nchini Indonesia wamepiga marufuku wanafunzi kusherekea siku ya wapendanao wakisema sherehe hizo zinachochea vijana kujihusisha na vitendo vya ngono kiholela.
Katika mji wa Makassar polisi walivamia majumba ya starehe na kuharibu mipira ya 'Condom' iliyowekwa kwa wazi.
Meya wa mji huo ameambia BBC kwamba mipira ya 'Condom', iliondolewa maeneo ya wazi baada ya wateja kulalamika na kusema inapatikana lakini haiwekwi wazi.
Katika mji wa pili mkubwa wa Surabaya, wanafunzi wameonywa dhidi ya kusherekea siku ya wapendanao na maafisa wa serikali ambao wamesema sherehe kama hiyo ni kinyume cha maadili ya jamii.
No comments:
Post a Comment