Zlatan Ibrahimovic amesema Manchester United wanaweza kunyanyua mataji matatu msimu huu wakati wapinzani wao wengi hawatapata chochote
Jose Mourinho hatapata fursa ya kurejea tena nafasi ya jana hadi Machi 4 watakapoikabili Bournemouth.
"Tunaendelea kusonga mbele," Ibrahimovic aliwaambia waandishi baada ya ushindi dhidi ya Watford.
"Tunataka kufanikiwa kwenye michuano ya Ligi ya Europa na kuwa na mechi nzuri dhidi ya St Etienne.
"Kutoka kwenye mataji matano msimu huu, tumetwaa moja [Ngao ya Jamii] na bado tunapigania manne.
"Nadhani katika timu nne za juu moja itakuwa bingwa wa Ligi.
"Zilizobaki hazitapata taji, lakini tunalo moja na tunaweza kupata la pili [Kombe la EFL], na bado tumo kwenye michuano ya Ligi ya Europa na Kombe la FA, kwa hiyo kama hatutakuwa mabingwa wa Ligi ya Uingereza, tunaweza kujaribu kutwaa mataji mawili au matatu."
Ibrahimovic amekiri kwamba taji la Ligi Kuu Uingereza liko nje ya uwezo wao kwa sasa, lakini amesisitiza kuwa timu yao ipo tayari kutumia fursa ya yeyote atakayeteleza.
"Tunajua kwamba tumekwama kwenye nafasi moja kwa muda mrefu," alisema.
"Tumeshika [nafasi ya tano] kwa dakika 20 labda na tumerudi kwenye nafasi ile ile tena, lakini tunajua tunachohitaji kufanya. Tunahitaji kuendelea kushinda kukwea nafasi za juu na tunatuma kwamba wengine watapoteza pointi na tutaweza kuwapita."
Ibrahimovic, 35, amekuwa mchezaji wa kwanza United kufunga magoli 20 tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu, lakini aliumia moyo kutofunga dhidi dya Watford.
No comments:
Post a Comment