Winga huyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga, tangu ajiunge nayo kwenye misimu minne na nusu iliyopita sasa anataka kwenda nje
Winga wa Yanga Simon Msuva amesema ataitumia michuano ya kimataifa, ili kujitangaza na kupata timu ya kucheza nje ya Tanzania.
Winga huyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga, tangu ajiunge nayo kwenye misimu minne na nusu iliyopita.
Msuva alisema, kuwa amekuwa akicheza kwa malengo tangu aanze kucheza soka la ushindani na kutokana na uzoefu alioupata akiwa na timu hiyo anaamini yupo tayari kucheza soka nje ya Tanzania.
“Nataka kuitumia michuano hii kwa sababu ndiyo inatoa fursa ya kuonekana zaidi kuliko ligi ya ndani ndiyo sababu nimedhamiria kuhakikisha mwaka huu naitumia mizuri ili niweze kutimiza ndoto yangu kwa kupata timu ya kucheza soka la kulipwa,” amesema Msuva.
Winga huyo ambaye hadi sasa ameifungia Yanga mabao 10 kwenye ligi inayoendelea hivi sasa , alisema anataka kuondoka Yanga baada ya kufanikiwa kubeba mataji yote ya ndani akiwa na timu hiyo ambayo jana ilitmiza miaka 82 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema kwa Afrika angependa kucheza soka Afrika Kusini, au DR Congo, na kwa Ulaya nchi yoyote ambayo anaamini kiwango chake kitakuwa kwa haraka na kusajiliwa na timu kubwa za mataifa ya Hispania,Italia, Ujerumani au Uingereza.
Winga huyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga, tangu ajiunge nayo kwenye misimu minne na nusu iliyopita.
Msuva akiwa na Yanga misimu miwili iliyopita aliweza kuibuka mchezaji bora na mfungaji bora wa ligi hiyo hayo yakiwa ni mafanikio makubwa kwake tangu alipotua timu hiyo ya Jangwani.
Kama atavutia klabu za nje kwa kiwango chake ni dhahiri atafuata nyayo za Mbwana Samatta anayekipiga Genk na Thomas Ulimwengu.
No comments:
Post a Comment